Thursday, April 5, 2012

News

9:17:00 AM - By Hisia 0


Kundi la wanamgambo la Al- Shabab limesema limehusika na shambulizi la bomu katika mji mkuu wa Somalia siku ya jumatano lililouwa watu nane wakiwemo wakuu wa mchezo wa mpira wa soka na Olimpic.
Shambulizi hilo lilitokea katika jumba la michezo lililofunguliwa tena hivi karibuni nchini humo . Mashahidi wanasema mwanamke mmoja alijilipua mwenyewe wakati waziri mkuu Abdiweli Mohamed Ali akihutubia mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiadhimisha mwaka mmoja wa televisheni ya taifa ya Somalia.
Waziri mkuu aliithibitishia VOA kwamba mwanamke huyo alifanya shambulizi na alielezea kuwa hilo ni tukio la kigaidi lililofanywa na Al- Shabab.
Shambulizi hilo limemuuwa mkuu wa kamati ya michezo ya Olimpic Adan Haji Yabarow Wiish na mkuu wa jumuiya ya mchezo wa soka Said Mohamed Nur.

Tags:
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Pellentesque volutpat volutpat nibh nec posuere. A die shopuf pogest concludi cum administrasset slushie intus calidum brioche.
Follow me @Bloggertheme9
Subscribe to this Blog via Email :

0 maoni:

Powered by Blogger.
back to top